Psalms 10

Sala Kwa Ajili Ya Haki


1
Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bKwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali?
Kwa nini unajificha wakati wa shida?


2 cKatika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,
waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

3 Hujivunia tamaa za moyo wake;
humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

4 dKatika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,
katika mawazo yake yote
hakuna nafasi ya Mungu.

5 eNjia zake daima hufanikiwa;
hujivuna na amri zako ziko mbali naye,
huwacheka kwa dharau adui zake wote.

6 fAnajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,
daima nitakuwa na furaha,
kamwe sitakuwa na shida.”

7 gKinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;
shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.

8 hHuvizia karibu na vijiji;
kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,
akivizia wapitaji.

9 iHuvizia kama simba aliye mawindoni;
huvizia kumkamata mnyonge,
huwakamata wanyonge na kuwaburuza
katika wavu wake.

10 jMateka wake hupondwa, huzimia;
wanaanguka katika nguvu zake.

11 kAnajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau,
huficha uso wake na haoni kabisa.”


12 lInuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu.
Usiwasahau wanyonge.

13 mKwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?
Kwa nini anajiambia mwenyewe,
“Hataniita nitoe hesabu?”

14 nLakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,
umekubali kuyapokea mkononi mwako.
Mhanga anajisalimisha kwako,
wewe ni msaada wa yatima.

15 oVunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,
mwite atoe hesabu ya maovu yake
ambayo yasingejulikana.


16 p Bwana ni Mfalme milele na milele,
mataifa wataangamia watoke nchini mwake.

17 qUnasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,
wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,

18 rukiwatetea yatima na walioonewa,
ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.
Copyright information for SwhKC